Kituo cha habari cha Europe1 kimeripoti kuwa, licha ya mashirika mengi ya Ulaya kuwataja watu waliohusika na shambulizi hilo kuwa ni kundi la watu wasiojulikana, lakini mashirika ya habari ya Palestina yamesema, Wazayuni wenye misimamo mikali walishambulia msikiti na Chuo Kikuu cha mji wa Birzeit katika Ukingo wa Magharibi na kuandika maneno machafu dhidi ya Waislamu, Uislamu na Mtume Muhammad SAW katika kuta zake.
Hii ni mara ya pili kwa Wazayuni wenye misimamo mikali kushambulia misikiti ya Ukingo wa Magharibi katika wiki hii. Mwanzoni mwa wiki Wazayuni hao waliushambulia Msikiti wa Dhu Nurein katika kijiji cha Qasra huko Nablos na kuuteketeza kwa moto. 857920