Waandamanaji hao wamelalamikia vikali msimamo wa Saudia kuhusu mapinduzi yao ya hivi karibuni waliyofanya dhidi ya dikteta Hosni Mubarak. Waandamanaji hao pia wamelalamikia vikali dharau iliyofanywa hivi karibuni na askari usalama wa Saudia dhidi ya raia wa Misri waliokwenda Saudia kutekeleza ibada ya Umra.
Askari usalama wa Misri waliingilia kati na kuwatawanya kwa nguvu waandamanaji ili kulinda ubalozi wa nchi hiyo mjini Cairo, jambo ambalo lilipelekea kujeruhiwa watu kadhaa katika ghasia hizo. Maandamano hayo yalifanyika sambamba na mengine kama hayo ambayo yalifanyika dhidi ya ubalozi wa utawala haramu wa Israel mjini Cairo.
Wiki iliyopita pia Wamisri walikusanyika mbele ya ubalozi wa Saudi Arabia na kuelezea malalamiko na kuchukizwa kwao na kitendo cha Saudi Arabia cha kuwavunjia heshima Wamsri na kutaka balozi wa nchi hiyo pamoja na utawala haramu wa Isreal wafukuzwe nchini humo mara moja. 857804