IQNA

OIC, UNESCO zajadili nafasi ya wanawake Waislamu duniani

14:52 - September 11, 2011
Habari ID: 2185046
Taasisi mbili za Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC zimeandaa kikao kuhusu nafasi ya wanawake Waislamu katika jamii.
Kikao hicho kimefanyika katika makao makuu ya UNESCO mjini Paris.
Mwaka jana kikao kuhusu maudhui hii kilinfanyika mjini Tehran na mwaka huu mzungumzaji wa kikao cha ufunguzi alikuwa ni Muirani ambaye aliangazia mafanikio ya wanawake nchini Iran hasa katika uga wa elimu.
Aidha washiriki wamejadili nafasi ya wanawake Waislamu katika mwamko unaoendelea katika nchi za Kiarabu. Washiriki pia wamejadili matatizo ya wanawake Waislamu kama vile kutopata nafasi za kujiendeleza, elimu, sheria za kibaguzi na kutopata fursa katika daraja za juu za kibiashara na kisiasa.
858225
captcha