Kesi hiyo ambayo inaingia kwenye siku yake ya tano leo inasimamiwa na Ahmad Rif'at.
Hosni Mubarak anahukumiwa pamoja na wanawe wawili na Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani Habib al Adili.
Kikao cha leo cha kesi ya dikteta wa Misri kimesikiliza ushahidi wa Mkuu wa Baraza la Kijeshi linalotawala Misri Muhammad Hussein Tantawi.
Katika kikao kilichopita cha kesi hiyo mahakama ilisikiliza ushahidi wa Meja Jenerali Hassan Abdul Hamid ambaye alisisitiza kuwa jeshi la polisi lilitumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji. 858615