Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC jana Jumapili ilitoa taarifa kwa mnasaba wa kukumbukwa matukio ya Septemba 11 nchini Marekani. Katika taarifa hiyo OIC imesisitiza kwa mara nyingine tena kwa niaba ya nchi wanachama wake 57 msimamo wake thabiti wa kupinga na kulaani kila aina ya ugaidi na utumiaji nguvu dhidi ya jamii ya mwanadamu.
Imesema kuwa kutokana na kuwa ugaidi unafanyika kwa mbinu tofauti duniani, hauwezi kuondolewa kwa kutumia njia za kijeshi tu, na kuongeza kuwa kuna haja ya kufanyika kila liwezekanalo ili kutambua sababu zinazopelekea kuenea kwa ugaidi duniani na pia kutafuta njia za kuondoa tofauti zinazopelea kudhidhiri tatizo hilo katika jamii ya mwanadamu.
Taarifa ya OIC imewataka wafuasi wa dini zote kuishi pamoja kwa amani na kuwataka wakabiliane na fikra zinazochochea mivutano ya kiutamaduni na ustaraabu duniani kufuatia mashambulio ya kigaidi ya Septemba 11 miaka 10 iliyopita.
Mashambulio hayo yamepelekea Waislamu kuandamwa na kukandamizwa kwa njia mbalimbali na nchi za Magharibi kwa madai ya kupambana na ugaidi duniani. 859064