Uzingatiwaji wa mafundisho ya Kiislamu kuhusiana na masuala kama vile utukufu wa mwandamu, uhuru, usawa, uadilifu, ihsani, uwajibikaji na utu ni jambo ambalo linasaidia katika kuimarisha haki za binadamu duniani.
Hayo yamesemwa na Kamran Hashimu mhadhiri katika Chuo Kikuu Huru cha Kiislamu cha Iran katika kongamano la Mazungumzo, Dini na Tamaduni za Asia lililomalizika hapa mjini Tehran siku ya Jumatatu.
Amesema haki za binadamu ni maudhui muhimu ya kimataifa na Waislamu ambao wana utajiri mkubwa wa kiutamaduni na thamani za kidini, wanapasa kuwa na nafasi muhimu katika kuainisha mkondo wake.
Hashimi amesema utajiri mkubwa wa kiutamaduni na kidini wa bara kongwe la Asia unaweza kutoa mchango mkubwa katika uimarishaji na uenezwaji wa haki za binadamu ulimwenguni. Mhadhiri huyo wa chuo kikuu amesema kuwa nchi nyingi za ulimwengu wa tatu zinalichukulia suala la haki za binadamu kuwa suala la kiusalama na kisiasa katika hali ambayo suala hilo linapaswa kuchukuliwa kuwa tatizo la kiutamaduni na kijamii. 859611