IQNA

Kushikamana na Qur’ani, nukta ya pamoja ya mwamko wa Kiislamu

18:39 - September 14, 2011
Habari ID: 2186861
Katibu wa Kongamano la Kimataifa la Mwamko wa Kiislamu amesema nukta ya pamoja ya mwamko wa Kiislamu katika nchi za eneo ni kufungamana na Qur’ani na kurejea katika thamani za Kiislamu zitokanazo na Qur’ani Tukufu.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Tehran siku ya Jumanne, Dr. Ali Akbar Velayati ameongeza kuwa hatua ya wanamapinduzi Misri kuuteka ubalozi wa utawala haramu wa Israel mjini Cairo ni nukta muhimu katika matukio ya eneo.
Dr. Velayati ambaye wakati moja alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa zaidi ya wasomi 600 kutoka nchi mbali mbali za dunia na ulimwengu wa Kiislamu watashiriki katika kongamano hilo la wiki ijayo pamoja na wasomi 400 wa ndani ya Iran.
Dr. Velayati amesema mapinduzi yanayojiri sasa katika nchi za Kiarabu yanashabihiana na mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ambayo sasa yanachukuliwa kuwa kigezo na wananchi wa eneo.

860284
captcha