Taarifa ya mwisho ya mkutano huo uliohudhuriwa na wasomi, wanafikra na maulamaa zaidi ya 600 kutoka zaidi ya nchi 110 duniani imesisitiza juu ya udharura wa kulindwa umma wa Kiislamu na umoja baina ya wafuasi wa dini hiyo. Washiriki katika mkutano huo wa kimataifa wamesema kuwa wimbi la sasa la mwamko wa Kiislamu ni matunda ya Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, mafunzo na miongozi ya hayati Imam Khomeini mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu na mafanikio makubwa ya wanamapambano wa Kiislamu huko Lebanon na Palestina. Taarifa hiyo imesema kuwa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bait sambamba na kuunga mkono mwamko wa Kiislamu wa wananchi wa Bahrain, inatangaza pia uungaji mkono wake wa pande zote kwa matakwa yao halali. Taarifa hiyo pia imelaani mauaji yanayoendelea kufanywa na makundi ya kigaidi yaliyobuniwa na Magharibi dhidi ya wananchi wa Iraq na Afghanistan. Vilevile imeunga mkono mapambano ya harakati ya Hizbullah ya Lebanon na kuitaja kuwa ni mstari wa mbele wa mapambano dhidi Wazayuni Maghasibu na ubebebru wa kimataifa. Taarifa ya Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bait pia imetoa wito wa kutolewa misaada zaidi kwa wananchi aliokumbwa na baa la njaa nchini Somalia. 861265