Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya jana mjini Tehran mesema madikteta wa eneo hili wameanguka kutokana na harakati za mwamko wa Kiislamu na kwamba suala hilo pia limeshadidisha harakati dhidi ya Marekani katika Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika.
Amesema, hatua ya kivitendo ya Waislamu wa Misri ya kuvamia ubalozi wa Israel na kumlazimisha balozi wa utawala wa Kizayuni kukimbia mji wa Cairo, na pia kukimbia balozi wa Israel huko Jordan kunaonyesha kubanwa sana utawala wa Kizayuni.
Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami vilevile amesema, Marekani imetetemeka baada ya wanamapinduzi kutangaza kuwa harakati zao ni za Kiislamu na ni kwa ajili ya kuunda tawala zinazochaguliwa na wananchi.
Hatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran pia ameelezea matumaini yake kuwa mwamko wa Kiislamu utaendelea hadi pale madikteta wote hasa wa eneo hili watakapoangushwa.
861599