IQNA

Harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Misri yaikosoa Uturuki

10:21 - September 17, 2011
Habari ID: 2188112
Harakati ya Ikwanul Muslimin ya Misri imeikosoa Uturuki kwa kuingilia mambo ya ndani ya nchi hiyo.
Msemaji wa Ikwanul Muslimeen Mahmoud Ghazlan amelalamikia vikali pendekezo la Waziri Mkuu wa Uturuki Rajab Tayyib Erdogan ambaye amewataka watu wa Misri waunde dola ya kisekula au isiyo ya kidini. Ikhwanul Muslimin imesema matamshi hayo ya Erdogan ni uingiliaji wa mambo ya ndani ya nchi hiyo.
Weledi wa mambo wanaamini kuwa matamshi ya Erdogan ni pigo kwa harakati ya Ikwanul Muslimin ambayo inataka kushriki katika uchaguzi ujao nchini Misri. 861687
captcha