Akizungumza kupitia Televisheni ya Kitaifa ya Syria jasusi huyo mwenye uraia wa Jordan na Palestina amesema aliusaidia utawala haramu wa Israel katika kumuua kamanda huyo wa ngazi za juu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon. Mughniya aliuawa shahidi mjini Damascus.
Aidha jasusi huyo amekiri kuwapa majasusi ya Israel habari kuhusu maeneo kadhaa ya kisiri nchini Syria.
Katika miezi ya hivi karibuni Syria imekuwa ikikumbwa na machafuko na serikali ya Damascus inasema majasusi wa kigeni wanatoa misaada kwa magenge ya watu wenye silaha wanaolenga raia. Hadi sasa watu 1,600 wameuawa katika machafuko hayo.
Syria imesema maafisa usalama wake wapatao 700 wameuawa katika mapigano na mgenge hayo ya kigeni ambayo aghalabu yanapata msaada wa utawala haramu wa Israel.
862765