IQNA

Iran kugawa Misahafu 97000 miongoni mwa Mahujaji

15:19 - September 18, 2011
Habari ID: 2189259
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuwa itagawa nuskha 97000 za Qur'ani Tukufu miongoni mwa Mahujaji Wairani mwaka huu.
Haya ni kwa mujibu wa afisa mwandamizi wa Hija nchini Hujatul Islam Hamid Ahmadi. Amesema Misahafu hiyo itakuwa na tarjumi ya Kifarsi ya Ayatullah Makarim Shirazi.
Ameongeza kuwa Mahujaji wote Wairani watapokea zawadi ya Msahafu kabla ya kuanza safari yao ya kimaanawi.
Hujjatul Islam Ahmadi ameendelea kusema kuwa Misahafu hiyo itachapishwa kwa makaratasi ya kiwango cha juu.
862708
captcha