Mahmud Muzaffar Mkuu wa Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema tayari jumuiya hiyo imeshatuma shehena 14 kwa ajili ya Wasomali wanaokumbwa na njaa Afrika Mashariki.
Amesema shehena hizo zinajumuisha, vyakula, dawa, mahema, vifaa vya tiba na vitu vingine vya dharura.
Mozaffar amesema Iran ina kambi sita katika mji mkuu Mogadishu pamoja na hospitali ya muda inayotoa huduma mjini humo.
Hadi sasa wananchi wakarimu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wametoa misaada ya zaidi ya dola milioni 350 kwa ajili ya kuwasaidia ndugu za wa Somalia.
862312