IQNA

Wazayuni washambulia Msikiti wa al Aqsa

9:37 - September 19, 2011
Habari ID: 2189670
Kundi la Wazayuni lililokuwa likisaidiwa na askari wa Israel jana Jumapili lilivamia Msikiti wa al Aqsa kupitia mlango wa magharibi wa msikiti huo mtakatifu.
Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa kundi la Wazayuni lilishambulia msikiti huo wakati Waislamu walipokuwa wakaitekeleza ibada ya Sala ndani ya msikiti.
Tangazo lililokuwa limetolewa na Wazayuni kwamba watavamia msikiti huo liliwafanya Waislamu wakusanyike kwa wingi katika eneo hilo takatifu kwa ajili ya kulilinda.
Mpango wa kuvamia msikiti wa al Aqsa ulitangazwa katika kongamano lililotayarishwa na utawala wa Kizayuni wa Israel chini ya kisingizio cha kukarabati msikiti huo.
Utawala huo ghasibu pia umepeleka idadi kubwa ya askari wake katika milango yote ya kuingilia Masjidul Aqsa. 863249


captcha