Amesema juhudi hizo zimewatia moyo wananchi wa Palestina kwa ajili ya kuendelea kupigania haki na dini yao tukufu.
Hayo yalisemwa jana Jumapili na Ahmad Jibril, Katibu Mkuu wa PLO katika kikao cha kwanza cha Mwamko wa Kiislamu kilichofanyika mjini Tehran kuanzia siku ya Jumamosi. Amesema kwa miaka mingi sasa madola ya kibeberu ya Magharibi yamekuwa yakipotosha hali ya mambo katika ardhi za Wapalestina zinazoendelea kukaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel na kuongeza kwamba, Waislamu wana jukumu zito la kurekebisha hali hiyo na kuzifahamisha jamii za Magharibi hali halisi ya ardhi hizo.
Huku akisisitiza kwamba Nchi za Magharibi na Wazayuni wamelenga moyo wa ulimwengu wa Kiislamu yaani Palestina na Quds Tukufu, Jibril amewataka wanazuoni na viongozi wa nchi za Kiislamu kuhimiza na kuwapa moyo zaidi Wapalestina katika mapambano yao dhidi ya maadui wao.
Ameshangazwa na baadhi ya wanazuoni wa Kiislamu ambao wamekuwa wakishajiisha na kuunga mkono siasa za NATO na Marekani katika nchi za Kiislamu, pande mbili ambazo zimekuwa zikiua Waislamu kwa umati katika nchi hizo zikiwemo za Iraq, Afghanistan na Somalia. Amesema Syria ni miongoni mwa nchi chache ambazo zimebaki katika mstari wa mbele wa mapambano ya Wapalestina dhidi ya utawala haramu wa Israel kufuatia uchokozi wake wa mwaka 1982. Amewataka Waislamu wote kuwa macho na kutoruhusu Wamagharibi na Wazayuni kuzidhibiti zaidi nchi za Kiislamu na kuteka nyara mapinduzi ya wananchi dhidi ya tawala za kidikteta. 863440