Ameongeza kuwa maadui wanafanya kila wawezalo ili kuzusha mgawanyiko kwa kutangaza kuweko hitilafu kati ya wananchi wa Iran, Misri na Saudi Arabia. Dakta Mahmoud Ahmadinejad Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Jumapili katika marasimu ya kufunga Kikao cha Kimataifa cha Mwamko wa Kiislamu hapa Tehran kuwa walimwengu hawaridhishwi na hali ya ulimwengu ilivyo sasa na kwamba wananchi wa Marekani na Ulaya pia hawaridhishwi na hali hiyo.
Amesema mwamko wa Kiislamu katika nchi za Kiislamu na maeneo mengine ya dunia unapaswa kuuimarishwa ili kufikia malengo yake ya mwisho.
863413