IQNA

Jumuiya ya Kimataifa ya Mwamko wa Kiislamu kuanzishwa Tehran

15:21 - September 19, 2011
Habari ID: 2189942
Katibu wa Kongamano la Kimataifa la Mwamko wa Kiislamu lililomalizika Jumapili hii mjini Tehran amesema Jumuiya ya Kimataifa ya Mwamko wa Kiislamu itaanzishwa.
Ali Akbar Velayati amesema jumuiya hiyo itakuwa na makao makuu yake mjini Tehran. Dr. Velayati ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo ya kimataifa ya Mwamko wa Kiislamu.
Mkutano wa kwanza wa Mwamko wa Kiislamu katika taarifa yake ya mwisho umesisitiza juu ya udharura wa kulindwa umoja na mshikamano wa umma wa Kiislamu.
Mkutano huo wa siku mbili uliofanyika hapa mjini Tehran umehudhuriwa na mamia ya wanafikra kutoka nchi za Kiislamu, Afrika, Ulaya na Marekani.
863664
captcha