IQNA

Umoja wa Afrika walitambau rasmi Baraza la Mpito la Libya

15:29 - September 21, 2011
Habari ID: 2191251
Umoja wa Afrika umetoa taarifa ukitangaza kwamba unalitambua rasmi Baraza la Mpito la Libya kuwa mwakilishi halali wa wananchi wa nchi hiyo.
Taarifa hiyo imesema kuwa umoja huo unaunga mkono juhudi za baraza lililotajwa za kurejesha utulivu nchini na kuyashirikisha makundi yote ya kisiasa ya Libya katika jitihada za kubuni serikali ya umoja wa kitaifa.
Taarifa hiyo pia imelitaka Baraza la Mpito kuzuia kulengwa wafanyakazi kutoka nchi jirani waliokuwa wakifanya kazi katika sekta tofauti za nchi hiyo wakati wa serikali ya dikteta Muammar Gaddafi.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Afrika Kusini ambayo imekuwa na uhusiano mkubwa na dikteta huyo imesema kuwa itakata uhusiano huo na kutambua rasmi pamoja na kushirikiana kwa karibu na Baraza la Mpito la Libya. 864987
captcha