IQNA

Iraq yaituhumu Saudi Arabia kwa kutuma magaidi nchini humo

15:58 - September 21, 2011
Habari ID: 2191254
Kiongozi mmoja wa Iraq ameutuhumu utawala wa Aal Saud wa nchini Saudia kwamba unatuma nchini humo magaidi ambao wanaua watu wanaoyatembelea maeneo matakatifu kwa ajili ya kufanya ibada.
Akibainisha suala hilo, Farouq al-A'raji, Mkuu wa Idara ya Kamanda Mkuu wa Majeshi ya Iraq amesema kuwa magaidi wanaotekeleza vitendo vya umwagaji damu dhidi ya Wairaqi wanatoka katika nchi kadhaa za Kiarabu na hasa Saudi Arabia, magaidi ambao lengo lao kuu ni kuzusha vurugu na machafuko nchini humo.
Akiashiria rekodi mbaya ya Saudi Arabia ya kuchochea na kuunga mkono ugaidi na machafuko ya kimadhehebu nchini Iraq, al-A'raji amesema kwamba magaidi ambao walihusika na mauaji ya watu 22 hivi karibuni nchini Iraq walitoka katika nchi kadhaa za Kiarabu na hasa Saudia. Amesema ushahidi unathibitisha kwamba magaidi hao waliingia Iraq kwa msaada wa utawala wa Saudi Arabia.
Amesema licha ya uchochezi wote wa kimadhehebu na kikabila unaofuatiliwa na Saudi Arabia nchini Iraq, lakini wananchi wa nchi hiyo wamesimama imara na kwamba hawataruhusu umoja wao wa kitaifa kuvurugwa na wageni wasiowatakia mema. 864757
captcha