IQNA

Iran yalaani mauaji ya Rabbani

15:54 - September 21, 2011
Habari ID: 2191296
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametoa mkono wa pole kwa wananchi na serikali ya Afghanistan kufuatia kuuawa shahidi Rais wa zamani wa nchi hiyo Burhanuddin Rabbani.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametoa mkono wa pole kwa wananchi na serikali ya Afghanistan kufuatia kuuawa shahidi Rais wa zamani wa nchi hiyo Burhanuddin Rabbani.
Rabbani aliuawa jana katika mlipuko mkubwa uliotokea nyumbani kwake karibu na ubalozi wa Marekani mjini Kabul.
Ramin Mehmanparast Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani mauaji hayo ya kigaidi na kueleza kuwa kuuawa shahidi Burhanuddinn Rabbani aliyekuwa Mkuu wa Karaza kuu la Amani la Afghanistan sambamba na maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Amani kunaonyesha namna ugaidi ulivyoimarika huko Afghanistan, licha ya kuweko vikosi vya kigeni kwa muda wa miaka kumi kwa kisingizio cha kutaka kurejesha amani, uthabiti na utulivu nchini humo.
Burhanuddin Rabbani ambaye alikuwa mmoja wa marafiki wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na shakhsia aliyepinga kutiwa saini mkataba wa kiusalama kati ya Afghanistan na Marekani, aliuawa shahidi jana usiku nyumbani kwake katika eneo la Wazir Akbarkhan mjini Kabul.
864997
captcha