Mara hii hata waitifaki wa utawala huo katili wameshindwa kunyamaza kimya. Marekani ambayo ni muungaji mkono mkubwa wa dikteta Saleh imetoa taarifa na kulaani mauaji ya waandamanji 50 nchini Yemen. Uingereza, Ufaransa na Russia pia ni kati ya nchi zilizolaani ukatili huo wa Saleh.
Hivi karibuni pia mgombea katika uchaguzi ujao wa Rais huko Misri alikosoa msimamo wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na ulimwengu wa Kiislamu mbele ya jinai zinazofanywa na utawala wa Ali Abdallah Saleh dhidi ya wananchi wa Yemen.
Zaidi ya watu 50 waliuawa na wengine wasiopungua 100 kujeruhiwa katika hujuma iliyofanywa na vikosi vya Saleh siku ya Jumatatu mjini Sana’a na Taez.
Saudi Arabia ambayo inajulikana kama mtekelezaji wa njama za kibeberu za Marekani katika eneo hili la Mashariki ya Kati ingali inaendelea kufanya kila iwezalo kuhakikisha tawala za kidikteta za eneo hili zikiwemo za Bahrain na Yemen zinaendelea kubakia madarakani na kwa njia hiyo kufelisha harakati za mapinduzi ya umma katika nchi hizo.
864381