Zaidi ya viongozi 300 wa Waislamu, wasomi na wanazuoni wanatazamiwa kushiriki katika mkutano wa kila mwaka wa Kiislamu wa Jumuiya ya Waislamu Duniani (Muslim World League) katika mji mtakatifu wa Makka.
Mkutano huo utakaofanyika katika msimu wa Hija unatazamiwa kujadili masuala muhimu katika ulimwengu wa Kiislamu.
Mkutano huo ni wa 12 ulioandaliwa na Jumuiya ya Waislamu Duniani, amesema Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo Abdullah Al Turki. Ameongeza kuwa masuala kama vile da’awa ya Kiislamu na mapendekezo ya kuistawisha yatajadiliwa.
Kongamano hilo la siku nne litakuwa na vikao mbalimbali vitakavyojadili masuala kama vile umuhimu wa da’awa, changamoto, mbinu za da’awa n.k yatajadiliwa. Aidha kikao hicho kitajadili hali ya Waislamu katika nchi zisizokuwa za Kiislamu.
864625