Masuala muhimu yatakayojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na mchango wa vyombo vya habari vya Kiislamu katika kutetea harakati za mwamko wa Kiislamu na matakwa ya wananchi, udharura wa vyombo vya habari vya Kiislamu kutilia maanani wasiokuwa Waislamu, umuhimu wa kutumiwa mtandao wa intaneti katika kazi ya upashaji habari na kadhalika.
Kandokando ya mkutano huo kunafanyika kikao cha Masoko ya Filamu za Kiislamu ambacho kinashirikisha kazi mpya 700 kutoka mashirika na makampuni 90 wanachama. 866803