IQNA

Warsha ya mafunzo ya kuhifadhi nakala za maandiko ya kale kufanyika Guinea Bissau

15:19 - September 25, 2011
Habari ID: 2192948
Warsha ya mafunzo ya kuhifadhi nuskha za Kiislamu imepangwa kuanza kesho tarehe 26 hadi 30 Septemba huko Bissau mji mkuu wa Guinea.
Kituo cha habari cha Shirika la Elimu, Sayansi na Utamadu la Kiislamu ISESCO kimeripoti kuwa lengo la warsha hiyo ni kuchunguza mbinu za kisasa za kuhifadhi na kulinda nakala za maandishi ya kale za Kiislamu.
Ofisi ya mwakili wa ISESCO huko Bissau ndiyo inayoseimamia warsha hiyo.
Papa Toumane Ndiaye ambaye ni mtaalamu wa ISESCO anawakilisha shirika hilo katika warsha hiyo. 866823


captcha