IQNA

Kaburi la umati lagunduliwa Tripoli Libya

14:13 - September 26, 2011
Habari ID: 2193429
Khalid Sharif, Msemaji wa Baraza la Kijeshi la Libya mjini Tripoli, mji mkuu wa Libya ametangaza habari ya kugunduliwa kaburi moja la umati lililokuwa na mabaki ya miili 1700 pambizoni mwa mji huo.
Akizungumzia suala hilo mbele ya waandishi habari hapo jana tarehe 25 Septemba Sharif amesema kwamba kaburi hilo liligunduliwa baada ya kufuatilia ushahidi kutoka vyanzo tofauti. Amesema wahanga wa mauaji hayo walitendewa unyama wa kutisha, kwa kadiri kwamba miili yao ilimwagiwa mada fulani ili kuiharibu kabisa na kutojulikana.
Kwa mujibu wa ripoti za jumuiya za haki za binadamu, utawala wa Gaddafi uliua kwa umati mamia ya wafungwa mwaka 1966.
Salim al-Farjani mwanachama wa kamati ya kitaalamu inayochunguza jinai za Gaddafi amesema kuwa walipofika sehemu ya kaburi hilo walishangazwa kuona vipande vidogovidogo vya mabaki ya mifupa ya wahanga hao wa mauaji ya umati. Ameomba msaada wa mashirika ya kimataifa katika uwanja huo kwa sababu mabaki ya wahanga hao ni mengi mno ambayo hayawezi kushughulikiwa katika wakati unaofaa bila ya msaada kutoka nje. 867272
captcha