Dkt. Muhammad Husseini amesema hayo katika hafla ya ufunguzi wa duru ya tatu ya soko la filamu za Kiislamu ambayo inafanyika kwa mnasaba wa Kikao cha Tano cha Muungano wa Idhaa na Televisheni za Kiislamu hapa mjini Tehran.
Aidha amezitaka idhaa na televisheni za Kiislamu kubainisha utambulisho halisi wa Wamagharibi.
Waziri Husseini amesema, Wamagharibi wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali ikiwemo sanaa, radio na televisheni kwa ajili ya kufikia malengo yao machafu ya kuipotosha jamii kimaadili.
Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu wa Iran amesisitiza kwamba, jukumu la vyombo vya habari katika Ulimwengu wa Kiislamu ni kubwa mno hii leo hasa kutokana na kuongezeka njama za maadui dhidi ya Uislamu na Waislamu. Aidha Husseini ameashiria matukio ya Afghanistan, Iraq na Libya na kukosoa vikali siasa za Marekani na Shirika la Kijeshi la nchi za Magharibi NATO.
867130