Maudhui mbalimbali kuhusu muungano huo zitajadiliwa katika kikao hicho kitakachoendelea hadi Septemba 28.
Katika ufunguzi wa kikao hicho, Ali Karimiyani Katibu Mkuu wa Muungano wa Redio na Televisheni za Kiislamu ametoa pongezi kwa muungano huo kwa kukamilisha mwaka wa 5 na kusema kuwa, leo hii una wajumbe 200 kutoka nchi 32 duniani, na idadi hiyo inafanya muungano huo kuwa moja ya taasisi kubwa zaidi za vyombo vya habari duniani.
Karimiyan amesisitiza kwamba, miongoni mwa matunda ya muungano huo ni ushirikiano wa kuvutia na kutia moyo kuhusu matukio mbalimbali duniani, hasa jinsi matakwa ya wananchi yanavyotiliwa maanani wakati huu muhimu wa wimbi la mwamko wa Kiislamu katika nchi za Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika. 867400