IQNA

Aliyepanga mauaji ya Rabbani atiwa nguvuni Afghanistan

15:43 - September 26, 2011
Habari ID: 2193703
Vyombo vya usalama vya Afghanistan vimetangaza kuwa mtu aliyepanga mauaji ya kigaidi dhidi ya rais wa zamani wa nchi hiyo Burhanuddin Rabbani ametiwa nguvuni.
Naibu Mwenyekiti wa Kituo cha Upashaji Habari cha Afghanistan amesema kuwa mtu huyo anajulikana kwa jina la Hamidullah na anashikiliwa na kikosi cha usalama.
Sifatullah Sahhafi amesema kuwa habari zaidi kuhusu kadhia hiyo zitatangazwa baadaye.
Burhanuddin Rabbani aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Amani la Afghanistan aliuawa Jumanne iliyopita katika shambulizi ya bomu. Mtu aliyetekeleza mauaji hayo alidai kuwa alikuwa akitaka kufanya mazungumzo na Ustadh Rabbani kuhusu masuala ya amani nchini Afghanistan.
Rais Hamid Karzai wa Afghanistan jana alitoa amri ya kufanyika uhakiki kuhusu mauaji ya shakhsia huyo mkubwa. 867531

captcha