Wanamapinduzi wa Libya wanasemekana kuwa wamekaribia katikati mwa mji huo ambapo mapigano makali yanaendelea kati yao na wapiganaji waaminifu kwa Muammar Gaddafi. Mapema leo wanamapinduzi wa Libya waliteka na kudhibiti bandari muhimu ya Sirte.
Wakati huo huo Muammar Gaddafi aliyeko mafichoni amesema katika mkanda wa sauti uliorushwa hewani leo kupitia redio ya Bani Walid kwamba bado yuko Libya na anatarajia kwamba atafia katika ardhi ya nchi hiyo. Amewahimiza wapiganaji watiifu kwake kuendelaza mapigano na kwamba atakuwa nao bega kwa bega. 868593