IQNA

Iran kuwavutia watalii Waislamu

7:28 - September 29, 2011
Habari ID: 2195280
Iran ina nafasi kubwa ya kustawisha utalii wa kidini kutokana na nafasi yake ya kipekee na ya kidini.
Kuna maeneo matakatifu zaidi ya 8900 kote katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambapo 4300 miongoni mwa maeneo hayo yamesajiliwa katika orodha ya Kitaifa ya Turathi.
Maeneo hayo mengi mbali na kuwa na umuhimu wa kidini pia ni vivutio vya kiutamaduni na kihistoria.
Hata hivo mbali na Haram Takatifu ya Imam Ridha AS katika mji wa Mash'had na Haram ya Hadhrat Masouma katika mji wa Qum, maeneo mengine ya kidini hayajazingatiwa ipasavyo kwa mtazamo wa uwekezaji wa miundo mbinu kama vile mahoteli na usafiri.
Katika utamaduni wa Kiislamu, kusafiri kunahimizwa kwani humsaidia mwanadamu kufikia ukamilifu. Qur'ani Tukufu, katika aya mbalimbali kama vile sura Aal Imran aya za 137-138, Tawba aya ya 42, Yunis, aya ya 22, Nahl aya ya 80, An'am aya ya 11, Yusuf aya za 109-111, Ankabut aya ya 20 na Rum aya za 9-10, inahimiza na kusisitiza umuhimu na faida za safari.
868386
captcha