Ayatullah Muhammad Ali Taskhiri amesema, kwa msingi huo mkutano wa kukurubisha pamoja madhehebu ya Kiislamu na mwamko wa Kiislamu utafanyika mwanzoni mwa mwezi wa Dhilhija katika mji mtakatifu wa Makka.
Ayatullah Taskhiri ameashiria mwamko wa Kiislamu katika eneo la Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika na akasema kuwa kadiri shughuli za kukurubisha pamoja madhehebu ya Kiislamu zinavyoshika kasi zaidi ndivyo uwanja wa mwamko wa Kiislamu unavyotayarishwa zaidi kwani moja ya sifa za mwamko wa Kiislamu ni kufanya juhudi za kuimarisha umoja na mshikamano wa Kiislamu.
Amesema kuwa mkutano wa kukurubisha pamoja madhehebu ya Kiislamu na mwamko wa Kiislamu wa Makka utafanyika tarehe 2 au 3 Dhilhija na kwamba vitabu kuhusu mwamko wa Kiislamu vya hotuba za Imam Khomeini vitagawanywa kati ya hadhirina.
Ameongeza kuwa shakhsia kutoka nchi mbalimbali wataalikwa kushiriki katika mkutano huo na kubadilishana mawazo kuhusu maudhui hio. 871438