IQNA

Mtoto wa Mufti wa Syria auawa

15:08 - October 03, 2011
Habari ID: 2198147
Mtoto wa Mufti wa Syria ambaye katika siku za hivi karibuni amekuwa akibainisha wazi msimamo wake wa kuunga mkono serikali ya nchi hiyo na umoja wa taifa hilo, aliuawa jana Jumapili na magaidi.
Kwa mujibu wa shirika rasmi la Syria SANA Sariya Ahmad Badru Deen Hassun mwana wa Ahmad Badru Deen Hassun aliuawa jana na genge moja la kigaidi alipokuwa katika eneo moja la mji wa Saraqib. Licha ya juhudi za madaktari za kujaribu kuokoa maisha yake mara tu baada ya kupigwa risasi, lakini hawakufanikiwa katika juhudi hizo kutokana na risasi hizo kusibu moyo, figo na mapafu yake. Aliaga dunia alipokuwa akifanyiwa upasuaji.
Magenge ya magaidi wanayoungwa mkono na nchi za Magharibi yamekuwa yakitekeleza vitendo vya ugaidi na machafuko nchini Syria ikiwa ni katika kutekeleza njama za mabwana zao wa kigeni za kutaka kuipindua serikali ya nchi hiyo. Magenge hayo yamekuwa yakitekeleza shughuli zao katika miji kadhaa ya Syria na hivyo kuvuruga kabisa usalama na uthabiti wa miji hiyo. 872249
captcha