IQNA

Wanaharakati wa haki za binadamu watiwa mbaroni Saudi Arabia

16:20 - October 04, 2011
Habari ID: 2198878
Askari usalama wa Saudi Arabia jana usiku waliwatia mbaroni wanaharakati kadhaa wa kutetea haki za binadamu katika mji wenye wakazi wengi wa Kishia wa al-Awamiya katika mkoa wa Qatif.
Ripoti zinasema kuwa, askari usalama hao walivamia mji huo na kuwakandamiza wakazi wake wakiwemo wazee na wanawake kwa ajili ya kuwashinikiza wawakabidhi watoto wao wanaoshukiwa kushiriki kwenye maandamano ya hivi karibuni dhidi ya utawala wa Saudia.
Kufuatia utiwaji mbaroni huo, wakazi wa mji huo waliyarushia mawe magari ya askari usalama kutokana na vitendo vyao vya mara kwa mara vya kuwatia mbaroni wanaharakati wa haki za binadamu katika maeneo yenye wakazi wengi wa Kishia.
Tukio hilo pia limepelekea wakazi kadhaa wa mji huo kujeruhiwa. 872928
captcha