IQNA

Magaidi wanataka Syria ipige magoti mbele ya Israel

16:40 - October 04, 2011
Habari ID: 2198885
Mufti Mkuu wa Syria amesema katika mazishi ya mwanawe kwamba magenge yanayotekeleza vitendo vya kigaidi nchini humo hayawalengi watu mahsusi bali yamelilenga taifa zima la Syria na kwamba wanataka nchi hiyo ipige magoti mbele ya utawala haramu wa Israel.
Mtoto wa mufti mkuu huyo aliyeuawa hivi karibuni na magenge ya kigaidi alizikwa jana Jumatatu. Mazishi ya Sariya Hassun yalihudhuriwa na matabaka mbalimbali ya wananchi wa Syria wakiweno viongozi wa kidini wanaharakati wa haki za binadamu na viongozi wa serikali.
Muhammad Abdu Sattar as-Sayyid, Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu wa Syria aliiwakilisha serikali na kukabidhi ujumbe wa rambirambi wa Rais Bashar al-Assad kwa familia ya Mufti Mkuu Ahmad Hassun.
Mufti huyo amesema kuwa watu wanaotekeleza ugaidi nchini Syria wanakosea wakidhani kuwa watafanikiwa kutekeleza njama zao dhidi ya serikali na hatimaye kuifanya nchi hiyo ipige magoti mbele ya utawala ghasibu wa Israel. 873024
captcha