IQNA

Uislamu kuwa chanzo cha kwanza cha sheria nchini Libya

13:25 - October 05, 2011
Habari ID: 2199513
Baraza la Mpito la Libya limetangaza kwamba dini tukufu ya Kiislamu itakuwa chanzo na marejeo ya kwanza ya utungaji sheria katika Libya mpya.
Taarifa ya baraza hilo imesema suala hilo ni la ndani na linawahusu Walibya wenyewe.
Imesisitiza kuwa Walibya wameafikia juu ya suala hilo na hakuna mtu yeyote anayeweza kuwatwisha Walibya maoni yake kuhusu suala hilo.
Vilevile viongozi hao wapya wa Libya wameahidi kuondoka madarakani baada ya kurejeshwa kikamilifu usalama nchini humo.
Mustafa Abdul Jalil Mkuu wa Baraza la Taifa la Mpito la Libya amesema kwamba yeye na Waziri Mkuu Mahmoud Jibril wataendelea kushika nafasi zao hizo hadi wanamapinduzi watakapoudhibiti mji wa Sirte. Lakini amehidi kwamba hawatoshika wadhifa wowote katika serikali ijayo.
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya kupita wiki kadhaa za majadiliano na jitihada kubwa za kuunda serikali mpya ya mpito ya Libya. 873198
captcha