Akizungumzia suala hilo Mahmoud Sanjur, mkuu wa kitengo cha utendaji cha benki hiyo amesema benki ya kwanza ya aina hiyo ilipewa kibali cha kuendesha shughuli zake mwezi Mei uliopita. Amesema kuwa wataalamu wa masuala ya kifedha na kiuchumi wa nchi hiyo wametabiri kwamba Oman itaingia katika hatua mpya ya ustawi wa Kiuchumi baada ya kuzinduliwa benki hiyo ya pili ya Kiislamu katika kipindi cha miezi michache ijayo.
Amesema serikali ya Oman itaendelea kufanya juhudi za kurekebisha sheria za baadhi ya benki za nchi hiyo ili ziende sambamba na sheria za Kiislamu.
Mahmoud Sanjur amesema benki ya al-Izz itaanza shughuli zake mwanzoni mwa mwaka ujao kwa raslimali ya dola milioni 259 za Marekani. 873931