Mashirika hayo yametoa msaada huo uli utumike katika ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi za Wapalestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala wa Israel katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Shirika la Uungaji Mkono kwa Israel la Uingereza pekee, tokea mwaka 2007 hadi sasa limeutumia utawala huo haramu pauni laki tatu za Uingereza kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika Ukingo wa Magharibi.
Inasemekana kuwa, mbali na misaada ya kifedha kwa ujenzi wa vitongoji vilivyotajwa, shirika hilo pia limekuwa likifadhili mafunzo ya kijeshi kwa askari wa Israel, askari ambao wamekuwa wakihusika katika vitendo mbalimbali vya jinai na mauaji dhidi ya Wapalestina wasio na hatia. 873869