Kikao cha uchunguzi huo ambao umedhaminiwa kwa ushirikiano wa chuo kikuu kilichotajwa na Chuo Kikuu cha Oxford kitafanyika mwanzoni mwa mwaka ujao.
Lengo la kufanyika kikao hicho cha siku tatu ni kunufaika na mbinu za masomo zilizotumika katika zama za kale kwa lengo la kuboresha viwango vya masomo katika vyuo vikuu. Uimarishaji wa mawasiliano na ushirikiano wa Magharibi na mashariki kwa madhumuni ya kunyanyua viwango hivyo vya masomo ni malengo mengine yatakayofuatiliwa katika kikao hicho.
Wanafikra na wasomi walio na hamu ya kushiriki kwenye kikao hicho wana muda wa hadi kufikia tarehe 15 Novemba wawe wameshawasilisha makala zao kwa sekritarieti ya kikao hicho. 876079