Kituo cha habari cha Islam Today kimeripoti kuwa maonyesho hayo yanafanyika kwa hima ya Muungano wa Kiutamaduni wa Uturuki na ubalozi wa nchi hiyo mjini Roma kwa lengo la kukurubisha pamoja Waislamu na Wakristo.
Maonyesho hayo yanafanyika katika Kasri ya Cancelleria huko Vatican na baada ya hapo yatahamishiwa katika miji mingine ya Ulaya.
Kazi zinazoonyeshwa katika maonyesho hayo zinaakisi sira na mwenendo wa Mtume Muhammad (saw).
Katika maonyesho hayo pia kuna tasbihi zilizotengenezwa na wasanii wa Kituruki. 880531