Televisheni ya al Alam imeripoti kuwa askari wa utawala wa Saudia wameendeleza mwenendo wa kukamata ovyo watu wa maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo na kuwapeleka katika vituo vya polisi na kikosi cha usalama.
Askari wa Saudi Arabia pia jana waliwafyatulia risasi na kuwajeruhi vijana wawili katika mji wa al Awamiya ambao sasa wamelazwa katika hospitali ya mji wa Qatif.
Ripoti zinazema kuwa wimbi la ukandamizaji na kuwafyatulia risasi raia wa maeneo ya mashariki mwa Saudi Arabia lilianza mwezi Februari mwaka huu baada ya eneo la al Awamiya kufanya maandamano ya kulaani uvamizi wa majeshi ya Saudia huko Bahrain na kudai haki zao za kiraia kama uhuru wakitaka pia kuachiwa huru wafungwa wa kisiasa. 885204