Shirika la habari la Saudi Arabia IINA limeripoti kuwa mkutano huo wa siku tatu unaofanyika chini ya anwani ya Kuhuisha Daraja za Mawasiliano kupitia Sayansi na Teknolojia, unachunguza taathira za matukio ya sasa ya ulimwengu wa Kiislamu na kutathmini athari zake katika medani za sayansi na teknolojia.
Masuala mengine yanayochunguzwa katika mkutano huo ni historia ya Kiislamu, uhusiano wa sayansi na masuala ya kiroho, elimu na siasa, teknolojia ya nano na kadhalika.
Mkutano huo unahudhuriwa na wasomi na wahadhiri wa vyuo vikuu kutoka nchi za Kiislamu kama Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Malaysia, Algeria, Azerbaijan, Bangladesh, Bosnia, Misri, Kuwait, Iraq, Morocco, Pakistan na nchi za Magharibi kama Marekani, Ujerumani, Australia, Canada na Ufaransa. 885056