Ikhwanul Muslimin na chama kingine cha upinzani cha Amal al Islami vilifanya kikao cha pamoja hivi karibuni na kuamua kutoshiriki katika serikali ya Waziri Mkuu mpya wa Jordan Awn Khasawneh. Taarifa ya pamoja iliyotolewa na vyama viwili hivyo vya upinzani inasema kwamba havikuridhishwa na jinsi waziri mkuu huyo alivyoteuliwa kuunda serikali mpya jambo ambalo limezusha shaka na dhana mbaya miongoni mwa wananchi wa nchi hiyo.
Tarehe 17 Oktoba Mfalme Abdallah II alimfuta kazi Waziri Mkuu wa zamani Maaruf Bakhit na kumuweka sehemu yake Awn Khasawneh. 885118