IQNA

Sheria za Kiislamu kuwa msingi wa utungaji sheria nchini Libya

15:21 - October 24, 2011
Habari ID: 2210991
Mustafa Abdul Jalil Mkuu wa Baraza la Mpito la Libya alisema jana Jumapili kwamba sheria za Kiislamu zitakuwa msingi muhimu wa utungaji sheria nchini Libya.
Akizungumza huko katika mji wa Benghazi katika sherehe za kutangaza kokombolewa kwa nchi hiyo kutoka mikononi mwa utawala wa kidikteta wa Mummar Gaddafi, Abdul Jalil amesema kuwa Libya ikiwa ni nchi ya Kiislamu itatunga sheria zake kutokana na mafundisho ya Kiislamu na kwa msingi huo sheria zote zilizokuwa zikitumiwa na utawala wa Gaddafi kupiga vita Uislamu zitafutwa.
Amezishukuru Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya kwa kuisaidia Libya kumwondoa madarakani Mummar Gaddafi.
Abdul Jalil pia amezungumzia mipango ya kuanzisha benki za Kiislamu nchini Libya hivi karibuni na kuongeza kuwa benki hizo hazitakuwa zikichukua wala kutoa riba na kwamba zitatekeleza shughuli zao kwa msingi wa mafundisho ya Kiislamu.
Amesema kwamba mapinduzi ya wananchi wa Libya yalianza kwa amani lakini yalikabiliwa na vitendo vya mabavu na nguvu kutoka kwa utawala wa dikteta Gaddafi. 885875
captcha