Kwa mujibu wa tovuti ya Nasij, Kabila hilo linalojulikana kwa jina la Qadhadhifa limetoa taarifa likisema kuwa mhusika mkuu wa kifo cha Kanali Muammar Gaddafi ni Sheikh Yussuf Qardhawi.
Taarifa hiyo imesema sheikh huyo alitoa fatuwa hiyo muda mrefu kabla ya kuuawa Gaddafi akihalalisha kifo chake, jambo lililowachochea wanamapinduzi kumuua, na kwa msingi huo ndiye anayepasa kubebeshwa lawama za kuuawa kwake.
Taarifa hiyo inaendelea kusema kuwa juhudi zote za kimataifa zitakazofanywa kwa ajili ya kutafuta mhusika halisi wa kifo cha Gaddafi zinapasa kuzingatia athari za fatuwa hiyo, la sivyo uchunguzi huo hautakuwa na maana. 886403