IQNA

Kikao cha habari cha Zawadi ya Kimataifa ya Mwamko wa Kiislamu kufanyika Tehran

17:20 - October 26, 2011
Habari ID: 2212471
Kikao cha kwanza cha habari cha Zawadi ya Kimataifa ya Mwamko wa Kiislamu kitafanyika jumamosi ijayo mjini Tehran.
Kikao hicho kitahudhuriwa na wajumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu akiwemo kiongozi wake Muhammad Baqir Khorramshad.
Kikao cha kwanza cha Zawadi ya Kimataifa ya Mwamko wa Kiislamu kitahusu sehemu tatu za postkadi, picha na vibonzo chini ya nara ya Mwamko, Hakika ya Dunia ya leo na Bishara ya Mustakbali Mwema.
Wasani wanatakiwa kuwasilisha kazi zao kwa sekretarieti ya zawadi hiyo ya kimataifa.
Washindi wa kwanza katika nyanja zote hizo watatunukiwa zawadi ya yuro 2500.
Muhula wa mwisho wa kutuma athari za wasanii kwa sekretarieti ya zawadi hiyo ni tarehe 3 Februari. 887869


captcha