IQNA

Kitengo cha kimataifa cha maonyesho ya magazeti mjini Tehran kufunguliwa Ijumaa

18:33 - October 26, 2011
Habari ID: 2212486
Kitengo cha kimataifa katika maonyesho ya kimataifa ya magazeti na masharika ya habari yanayoendelea mjini Tehran kitafunguliwa hapo siku ya Ijumaa.
Kitengo hicho katika maonyesho hayo ambayo ni ya 18 kitafunguliwa katika orofa ya pili ya Muswala wa Imam Khomeini (MA).
Maonyesho hayo ambayo hufanyika kila mwaka mjini Tehran hujumuisha wachapishaji wa magazeti na majarida pamoja na mashirika ya habari kutoka pembe mbalimbali za dunia.
Maonyesho ya mwaka huu yanayofanyika chini ya anwani ya 'Jihadi ya Kiuchumi, Ustawi wa Viwango Bora na Maadili ya Vyombo vya Habari' yalifunguliwa rasmi hapo siku ya Jumanne na yanatazamiwa kuendelea hadi tarehe Mosi Novemba. 887700
captcha