Kundi moja la wataalamu wa mambo ya kale kutoka nchi tofauti za dunia limeuandikia barua Umoja wa Mataifa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la umoja huo UNESCO likitaka hatua za lazima zichukuliwe na taasisi mbili hizo za kimataifa kwa shabaha ya kukabiliana na hatua ya utawala haramu wa Israel ya kutaka kujenga jumba la makumbusho ya kale kwa jina la Tasamuh juu ya makaburi ya kale ya Ma'manu Allah katika mji mtakatifu wa Quds.