Mkutano huo utahudhuriwa na Waziri wa Hija wa Saudi Arabia Fouad Abdul Salam na maulamaa kutoka nchi mbalimbali duniani.
Lengo la kongamano hilo limetajwa kuwa ni kubadilishana mawazo kuhusu jinsi ya kuarifisha zaidi utamaduni wa ibada hiyo ya kidini.
Katibu Mkuu wa kongamano hilo Hisham Balabbas amesema kuwa kongamano hilo kubwa la Hija hufanyika kila mwaka chini ya usimamizi wa Wizara ya Hija ya Saudia kwa lengo la kubainisha maana ya faradhi hiyo adhimu na katika kongamano hilo kunafanyika jitihada za kuwafahamisha Waislamu matunda na taathira za kiutamaduni za maulamaa wa Makka tangu zama za awali za Uislamu. 889215