Katika kikao chake cha Baraza Kuu kilichofanyika mjini Paris Ufaransa, shirika hilo liliipa Palestina uanachama huo kwa kura 107 za 'ndio' kutoka kura zote 180 zilizopigwa. Wanachama 50 wa baraza hilo walijizuia kupiga kura katika kikao hicho.
Ushindi huo wa Wapalestina katika shirika la UNESCO umekuja katika hali ambayo, Israel na Marekani ambayo ni mdhamini mkubwa wa bajeti ya shirika hilo, ilikuwa ikipinga vikali suala hilo, na hilo ni jambo lenye umuhimu mkubwa. Hii ni kwa sababu uanachama huo utaipa Palestina nafasi ya kutambuliwa rasmi katika taasisi nyingine muhimu za kimataifa.
Kabla ya hapo, Mahmoud Abbas, Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina alikuwa tayari amewasilisha ombi la kujiunga nchi yake na Umoja wa Mataifa ambapo Marekani imetishia kwamba itatumia kura ya veto kupinga jambo hilo. 890899