IQNA

Pazia la al Kaaba kubadilishwa siku ya Arafa

2:52 - November 02, 2011
Habari ID: 2216065
Pazia la Nyumba ya Mwenyezi Mungu al Kaaba ambalo limefumwa kwa kutumia hariri halisi na nyuzi zilizopakwa maji ya dhahabu litatundikwa juu ya nyumba hiyo tukufu katika siku ya Arafa.
Kwa sasa pazia hilo linatengenezwa katika kiwanda kinachoshona na kudarizi pazia la al Kaaba mjini Makka.
Mkuu wa karakana inayotengeneza pazia hilo Kamaluddin Sawadi amesema kuwa wataalamu kutoka maeneo yote ya Saudia wanashughulikia pazia hilo la al Kaaba katika karakana hiyo.
Amesema pazia hilo la al Kaaba linahitaji hariri na nyuzi nyingi zilizopakwa maji ya dhahabu na fedha. Ameongeza kuwa gharama za pazia la sasa la al Kaaba ni riale milioni 20 za Saudi Arabia. Amesema pazia hilo litawekwa juu ya al Kaaba tarehe 9 Dhulhija na lile la zamani litakwa vipande vipande ambavyo kwa kawaida hutolewa zawadi kwa shakhsia au jumuiya mashuhuri za Kiislamu. 891603

captcha